Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Njia 3 rahisi :Jinsi ya kutumia Facebook kutangaza na kukuza biashara yako

Ebu jiulize Leo, umeingia Facebook kwa mda gani?.. Asubuhi, mchana au jioni? Well, tafiti zinasema watu wengi hawana muda maalum, muda wowote akiwa free na simu yake, tayari ashaingia Facebook. Mfano rahisi tu, cheki kwenye daladala watu walioshika smartphone zao, huwezi kukosa ambao hawapo Facebook kwa muda huo. Au ingia Facebook ktk account yako, anytime lazima ukute watu wapo online, (jaribu hata sasa hivi !!) STORI ya hapo juu, ni funzo moja muhimu sana ambalo kama mfanyabiashara  au mjasiriamali wa karne hii ya teknolojia lazima ulifahamu. Na funzo lenyewe ni kutambua ATTENTION ya wateja wako wa sasa, na wa baadae walipo...na si sehemu nyingine unayoweza kuwafikia kiurahisi kama kupitia mitandao ya kijamii, yaani Facebook, Instagram, WhatsApp, Snapchat, YouTube n.k Kupitia social media, unao uwezo wa kufanya biashara yako 24hrs, kuongeza mipaka ya sehemu biashara yako inapoweza kufika...na hivyo kuleta faida kubwa sana kwako kama ukiitumia ipasavyo. Kuna stori kibao j
Machapisho ya hivi karibuni

JINSI YA KUKUZA BIASHARA NDOGO: Mambo 6 ya kuzingatia...(part 2)

Huu ni mwendelezo wa makala yetu iliyopita, tuna endelea na jambo la 4 #4. Kuhakikisha unatengeneza mtandao wako wa kukuza soko lako Tambua kuwa biashara hizi ndogo ndogo mara nyingi faida zake si kubwa sana lakini zina faida endapo utakua na masoko mengi tofauti tofauti. Na maanisha nini?? Usiwe unapika Crips ukataka uishie kuuza wewe mwenyewe au ukaishia kuuzia hapo kibarazani kwako Hakikisha unakuwa na waru wengine ambao watanunua kwako bidhaa hata kwa jumla na wao kwenda kuziuza au lah uwe na sehemu nyingi za kwenda kuuzia bidhaa zako. Unapika vitafunwa usiishie kuuza hapo kibarazani kwako, badala yake ongea na viduka vya Mangi waachie vitafunwa vyako hapo wakuuzie au uwauzie kwa jumlan tengeneza vingine tafuta sehemu zingine za kwenda kuuza kama ni maofisin, stendi, sehemu zenye msongamano wa watu, mahotelini au migahawani, nk ili soko lako liwe kubwa kusudi ukikusanya hizo mia mbili au mia tano sehemu nyingi zaidi zikuletee faida nzuri vinginevyo kwa kutegemea soko

JINSI YA KUKUZA BIASHARA NDOGO: Mambo 6 ya kuzingatia...(part 1)

Nimegundua kuwa watu wengi tunafanya biashara ndogo ndogo ila zinashindwa kuendelea au kukua au kusonga mbele kwa sababu kuna mambo machache aidha tunayafahamu ila tunayapuuza au hatuyajui Basi leo naomba nishee nanyi baadhi ya mambo ambayo naamini ni ya msingi sana tunapaswa kuyazingatia pindi tunapoanzisha biashara na mtaji mdogo na hii inaenda sambamba na sie hasa tunaofanya hizi biashara ndogo ndogo kwani mara nyingi huwa zinaanzishwa na mitaji midogo Ni mambo gani hasa ya msingi kuzingatia pindi unapoanza biashara na mtaji mdogo? Yafahamu haya mambo haya ya msingi ambayo ni muhimu kuyazingatia pindi unapoanzisha biashara yako kwa mtaji mdogo #1. Biashara iwe kwenye kitu ambacho unakijua vizuri au una uzoefu nacho Kama unaanza biashara kwa mtaji kidogo basi unahitaji kufanya biashara inayohusisha kitu ambacho wewe binafsi unakijua vizuri au una uzoefu wa kukifanya. Hii itakuwezesha wewe kuweka juhudi kwenye kufanya. Kwa sababu mtaji wako ni kidogo, huna muda wa ku

Mifano halisi: Masoko ya bidhaa zako za ujasiriamali (crips,tambi)

1.SHULENI (hasa za msingi) Kama ilivyo katika biashara ya Crips, Shule za Misingi pia ni Soko la Tambi za Dengu. Hapa katika Shule za Misingi pia kuna upenyo wa kufanya Biashara hii kwa kuuza Mwenyewe au kuwapa Vijana wakuuzie au kuwaomba wale wanaouza Vipipi wakuuzie kwa Kutengeneza Mgawanyo wa Pato la Kila bidhaa moja. Mfano Bidhaa ya Sh 200, Wewe mpe mtu uyo auze kisha mwambie achukue sh 40 na wewe utapata 160. Mara zote nasema Chukua kidogokidogo kwa Wengi, Nikimaanisha Kama utapeleka bidhaa zako katika shule 10 na kupata Faida ya Sh 50 kwenye Kila bidhaa moja na wewe umepeleka bidhaa 100 kila shule. Maana yake utakuwa umetengeneza Faida ya 5000 Mara shule 10 utakuwa na 50,000 kwa Siku hii. Tambi za Dengu zinalika Pia shule za Misingi. 2.MADUKA YA MTAANI Maduka ya Mitaani ni sehemu ya Soko la Tambi za Dengu. Je Mtaani kwako kuna Maduka Mangapi, Je Maduka yaliochangamka ni mangapi? Je Maduka gani yanamuingiliano wa Watu sana. Jambo la Msingi hapa Ni kuangalia Maduka Yaliyocha

Jinsi ya kufanya utafiti wa masoko, kwako wewe mjasiriamali

Katika kutambua fursa za kibiashara, ni lazima ujue kufanya utafiti mzuri wa masoko,..jifunze kitu katika stori hii ya kweli kutoka kwa mjasiriamali mmoja.. "Katika pita pita zangu leo nikakutana na muuza crisps Nikasema wacha nimuungishe mjasiriamali mwenzangu huku tukipiga stori za hapa na pale......... Kwanza nilianza kwa kumuuliza bei ya crisp na kisha nikampa hela na kununua ili niweze kubonga nae stor vizuri maana asikwambie mtu, ni ngumu kumdadisi mfanyabiashara ikiwa hamjazoeana wala hamfahamiani. Mtu anaweza akahisi unamchawia au unamletea nuksi au pengine unataka na wewe uje ufungie biashara kama hyo halafu uishie kuwa mshindani wake Nikanunua pakiti yangu nikawa nakula mdogo mdogo huku nikianza kupuga nae stori. Nilimuanzia mbali sana ili kuepuka kumfanya ashindwe kuniweka bayana juu ya hiyo biashara yake. Nilianza kwa kumuelezea juu ya biashara yangu ya karanga na changamoto zake baada ya Diamond Karanga kuibuka (huku nikiwa hata sijawai fanya biashara ya karang

Jinsi ya kupika crips (mwanzo hadi mwisho)

MAHITAJI YA KUPIKA CRIPS ZA VIAZI ü   Viazi ü   Mafuta ya Kula ü   Chumvi Au Pilipili ya Unga ü   Mashine ya Kukatia ü   Moto na Vyombo vya kupikia. HATUA ZA UPISHI WA CRIPS ZA Viazi Kwanza menya Viazi vyako na Viweke Kwenye Maji ambapo vitaoshwa. Chukua Mashine yako ya Kukatia na Ioshe na Maji kwanza. Kata kwanza Viazi vyako ili viweze kuwa kama Vipande viitwavyo Crips. Weka Mafuta kwenye Moto na hakikisha moto wako unawaka vizuri. Hakikisha Wakati unakata Viazi vyako vidondokee kwenye maji ili visigandane. Hakikisha mafuta yanapata moto ndio uweke Crips zako humo. Subiria kaa muda wa Dakika 7 hadi 10 kisha Geuza na baada ya muda mchache crips zako zitakuwa zimesha iva. Ipua na uweke kwenye chujio la Kuchuja mafuta. Hakikisha mafuta yanachujwa na crips iwe kavu ili wakati unaweka kwenye vifuko isitengeneze Umafuta ndani yake itakera. Weka Kwenye Besen kisha weka chumvi kwa Mbali na upepete ili ichanganyik

BIASHARA YA CRIPS, ANZA LEO KWA MTAJI WA 50,000.

BIASHARA YA CRIPS....PART 1 Biashara ya Crips ni Biashara unayoweza sema ni Ndogo kama utawekeza kwa Udogo lakini pia unaweza sema ni ya kati kama utawekeza kwa ukati wake. Hii ni biashara ambayo mtu anaweza kuwekeza kwa kua na sh 50,000. Ndio Mtaji wa Elfu Hamsini unatosha kabisa kumfanya mtu aianze Biashara hii. Mtu anaweza Sema Inakuaje Elfu hamsini Ikawa Mtaji, Ni Hivi Katika 50000. Toa 20000 ya Mashine, Kisha Toa 12000 Ya Debe Moja la Viazi kisha toa 10500 ya Lita 3 za Mafuta , Kisha toa 2000 Ya Mkaa na Utoe pesa Ya Vifuko ni Sh 1200 vya kufungia na Chumvi 300 na Pilipili ya unga 500. Wataalamu wa Hesabu, ukipiga haizidi elfu 50. Halafu watu wapo mtaani wanalalamika hawana Mitaji,wanaishia kubeti, mara biko, tatu mzuka.. Kumbe mitaji yao wanachangia kwenye Harusi na Sendoff.  Embu jiulize umeua Mitaji mingapi kwa kuchangia Harusi na Sendoff, kubeti, kucheza biko/tatu mzuka au kununulia nguo ya Sherehe alafu kesho yake unapiga mihayo na kusema Vyuma Vimekaza. H