Ruka hadi kwenye maudhui makuu

JINSI YA KUKUZA BIASHARA NDOGO: Mambo 6 ya kuzingatia...(part 1)

Nimegundua kuwa watu wengi tunafanya biashara ndogo ndogo ila zinashindwa kuendelea au kukua au kusonga mbele kwa sababu kuna mambo machache aidha tunayafahamu ila tunayapuuza au hatuyajui

Basi leo naomba nishee nanyi baadhi ya mambo ambayo naamini ni ya msingi sana tunapaswa kuyazingatia pindi tunapoanzisha biashara na mtaji mdogo na hii inaenda sambamba na sie hasa tunaofanya hizi biashara ndogo ndogo kwani mara nyingi huwa zinaanzishwa na mitaji midogo



Ni mambo gani hasa ya msingi kuzingatia pindi unapoanza biashara na mtaji mdogo?


Yafahamu haya mambo haya ya msingi ambayo ni muhimu kuyazingatia pindi unapoanzisha biashara yako kwa mtaji mdogo


#1. Biashara iwe kwenye kitu ambacho unakijua vizuri au una uzoefu nacho

Kama unaanza biashara kwa mtaji kidogo basi unahitaji kufanya biashara inayohusisha kitu ambacho wewe binafsi unakijua vizuri au una uzoefu wa kukifanya.

Hii itakuwezesha wewe kuweka juhudi kwenye kufanya. Kwa sababu mtaji wako ni kidogo, huna muda wa kujifunza kwa kujaribu na kuacha, wewe unataka hiko kidogo ulichonacho kilete tofauti, kilete kipato angalau kidogo cha kusukuma maisha yako au mahitaji yako.

Hivyo pendelea kufanya biashara inayohusisha kitu unachojua na una uzoefu nacho, itakupunguzia changamoto ambazo zinaweza kuathiri sana mtaji wako kidogo

Mfano hapa umeshapata ujuzi wa Crips tena bila gharama yeyote hii ina maana huu ujuzi kwako ni mali kubwa mno, hivyo ukiamua kuanzisha biashara kwa kutumia huu ujuzi ina maana kwako hakutokuwa na haja ya kutumia fedha nyingi sana pindi unapoanzisha biashara yako kwani tayari huo ujuzi unao ni wewe tu kuutumia ipasavyo

#2. Kuepuka gharama ambazo sio za msingi

Ukumbuke kuwa mtaji wako ni mdogo hivyo unapoingia kwenye biashara, kuna gharama nyingi sana unazohitaji kuingia.

Katika gharama hizi kuna ambazo ni za msingi na nyingine sio za msingi.

Gharama za msingi ni zile ambazo bila ya kuzitimiza biashara haiwezi kwenda. Gharama ambazo sio za msingi ni zile ambazo hata zisipotimizwa basi biashara inaweza kuendelea vyema.

Zijue gharama zako za msingi na zile ambazo sio za msingi. Na kwa kipindi cha mwanzo cha biashara yako, epuka gharama zote ambazo sio za msingi. Hakikisha mtaji kidogo ulionao unakwenda kwenye maeneo muhimu hasa ya biashara yako

Sio una mtaji mdogo unataka uanze kukodi fremu ya Laki Moja au Mbili, uajiri wafanyakazi wakuwalipa, sio kwamba hivyo vitu si vya msingi lahasha ila kumbuka mtaji wako ni mdogo hivyo kwa kipindi cha mwanzo hivyo vitu visiwe na kipaumbele kwako kiasi kwamba vikakukwamisha usianzishe biashara au biashara ife kwa kuwa tu gharama zilikuwa kubwa.

Mfano biashara hizi za Crips au Maandazi unaweza kuanza kwa kupikia nyumbani tu au geto kwako lakini uhakikisha unayaweka mazingira yako masafi kabla hujaanza kupika au kutengeneza bidhaa zako kiasi kwamba hata wateja wakija wanakuta unafanya biashara katika mazingira mazuri na masafi na hivyo ukaepuka gharama ya kwenda kukodi fremu ambayo ingekulia mtaji wako zaidi au kukukwamisha kutoianzisha hiyo biashaar kisa tu huna mtaji wa kutosha



#3. Mwambie kila unayemjua kuhusu biashara yako

Ukiwa na mtaji mdogo ni vigumu sana kusema utaweza kulipia matangazo ili uitangaze biashara yako.

Hivyo, njia rahisi na ya kwanza kabisa ya kutangaza biashara yako unayoanza kwa mtaji kidogo ni kuhakikisha kila mtu ambaye unamjua anajua kuhusu biashara yako, hata kama yeye hawezi kuwa mteja wako tambua kiwa anaweza kuwaambia wengine ambao wanaweza kuwa wateja wazuri.

Tumia mtandao ulionao kuanza kutengeneza wateja wa biashara yako.

Unapoanza biashara kwa mtaji kidogo unahitaji kuanza kutengeneza faida mapema hivyo tumia njia hizi kuitangaza kwa kasi zaidi

Una watu wangapi katika Phonebook yako?...magroup ya WhatsApp na fb je??...

#itaendelea sehemu ya 2, USIKOSE

Toa neno lolote juu ya mada hii,,,...#share

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

BIASHARA YA CRIPS, ANZA LEO KWA MTAJI WA 50,000.

BIASHARA YA CRIPS....PART 1 Biashara ya Crips ni Biashara unayoweza sema ni Ndogo kama utawekeza kwa Udogo lakini pia unaweza sema ni ya kati kama utawekeza kwa ukati wake. Hii ni biashara ambayo mtu anaweza kuwekeza kwa kua na sh 50,000. Ndio Mtaji wa Elfu Hamsini unatosha kabisa kumfanya mtu aianze Biashara hii. Mtu anaweza Sema Inakuaje Elfu hamsini Ikawa Mtaji, Ni Hivi Katika 50000. Toa 20000 ya Mashine, Kisha Toa 12000 Ya Debe Moja la Viazi kisha toa 10500 ya Lita 3 za Mafuta , Kisha toa 2000 Ya Mkaa na Utoe pesa Ya Vifuko ni Sh 1200 vya kufungia na Chumvi 300 na Pilipili ya unga 500. Wataalamu wa Hesabu, ukipiga haizidi elfu 50. Halafu watu wapo mtaani wanalalamika hawana Mitaji,wanaishia kubeti, mara biko, tatu mzuka.. Kumbe mitaji yao wanachangia kwenye Harusi na Sendoff.  Embu jiulize umeua Mitaji mingapi kwa kuchangia Harusi na Sendoff, kubeti, kucheza biko/tatu mzuka au kununulia nguo ya Sherehe alafu kesho yake unapiga mihayo na kusema Vyuma Vimekaza. H

Jinsi ya kupika crips (mwanzo hadi mwisho)

MAHITAJI YA KUPIKA CRIPS ZA VIAZI ü   Viazi ü   Mafuta ya Kula ü   Chumvi Au Pilipili ya Unga ü   Mashine ya Kukatia ü   Moto na Vyombo vya kupikia. HATUA ZA UPISHI WA CRIPS ZA Viazi Kwanza menya Viazi vyako na Viweke Kwenye Maji ambapo vitaoshwa. Chukua Mashine yako ya Kukatia na Ioshe na Maji kwanza. Kata kwanza Viazi vyako ili viweze kuwa kama Vipande viitwavyo Crips. Weka Mafuta kwenye Moto na hakikisha moto wako unawaka vizuri. Hakikisha Wakati unakata Viazi vyako vidondokee kwenye maji ili visigandane. Hakikisha mafuta yanapata moto ndio uweke Crips zako humo. Subiria kaa muda wa Dakika 7 hadi 10 kisha Geuza na baada ya muda mchache crips zako zitakuwa zimesha iva. Ipua na uweke kwenye chujio la Kuchuja mafuta. Hakikisha mafuta yanachujwa na crips iwe kavu ili wakati unaweka kwenye vifuko isitengeneze Umafuta ndani yake itakera. Weka Kwenye Besen kisha weka chumvi kwa Mbali na upepete ili ichanganyik

JINSI YA KUKUZA BIASHARA NDOGO: Mambo 6 ya kuzingatia...(part 2)

Huu ni mwendelezo wa makala yetu iliyopita, tuna endelea na jambo la 4 #4. Kuhakikisha unatengeneza mtandao wako wa kukuza soko lako Tambua kuwa biashara hizi ndogo ndogo mara nyingi faida zake si kubwa sana lakini zina faida endapo utakua na masoko mengi tofauti tofauti. Na maanisha nini?? Usiwe unapika Crips ukataka uishie kuuza wewe mwenyewe au ukaishia kuuzia hapo kibarazani kwako Hakikisha unakuwa na waru wengine ambao watanunua kwako bidhaa hata kwa jumla na wao kwenda kuziuza au lah uwe na sehemu nyingi za kwenda kuuzia bidhaa zako. Unapika vitafunwa usiishie kuuza hapo kibarazani kwako, badala yake ongea na viduka vya Mangi waachie vitafunwa vyako hapo wakuuzie au uwauzie kwa jumlan tengeneza vingine tafuta sehemu zingine za kwenda kuuza kama ni maofisin, stendi, sehemu zenye msongamano wa watu, mahotelini au migahawani, nk ili soko lako liwe kubwa kusudi ukikusanya hizo mia mbili au mia tano sehemu nyingi zaidi zikuletee faida nzuri vinginevyo kwa kutegemea soko