1.SHULENI (hasa za msingi)
Kama ilivyo katika biashara ya Crips, Shule za Misingi pia ni Soko la Tambi za Dengu. Hapa katika Shule za Misingi pia kuna upenyo wa kufanya Biashara hii kwa kuuza Mwenyewe au kuwapa Vijana wakuuzie au kuwaomba wale wanaouza Vipipi wakuuzie kwa Kutengeneza Mgawanyo wa Pato la Kila bidhaa moja.
Mfano Bidhaa ya Sh 200, Wewe mpe mtu uyo auze kisha mwambie achukue sh 40 na wewe utapata 160. Mara zote nasema Chukua kidogokidogo kwa Wengi,
Nikimaanisha Kama utapeleka bidhaa zako katika shule 10 na kupata Faida ya Sh 50 kwenye Kila bidhaa moja na wewe umepeleka bidhaa 100 kila shule. Maana yake utakuwa umetengeneza Faida ya 5000 Mara shule 10 utakuwa na 50,000 kwa Siku hii. Tambi za Dengu zinalika Pia shule za Misingi.
2.MADUKA YA MTAANI
Maduka ya Mitaani ni sehemu ya Soko la Tambi za Dengu. Je Mtaani kwako kuna Maduka Mangapi, Je Maduka yaliochangamka ni mangapi? Je Maduka gani yanamuingiliano wa Watu sana.
Jambo la Msingi hapa Ni kuangalia Maduka Yaliyochangamka,yenye Muingiliano mkubwa wa watu. Hapo utapiga pesa .
Mfumo mzuri ambawo wote mtanufaika ni Huu hapa Kwa Bidhaa ya Tambi za Dengu ya Sh 500 Waambie wauze kwa 450 ili Hamsini ibaki dukani au unaweza kukubaliana nawo hata ukaicha sh 100 dukani na wewe ukachukua sh 400.
Ngoja nikwambie kitu kimoja, Unapotumia Mfumo wa Mauzo shirikishi Usiangalie sana kutengeneza pesa kwa mtu mmoja au kituo kimoja, Hapana wewe angalia utatengeneza sh ngapi kwa Maduka 10. Kama utapata faida sh 200 katika kila bidhaa maana yake utafaida nyingi kwa maduka yako mengi uliyoyasambazia bidhaa zako.
Ngoja nikukumbushe, Kwenye Biashara ndogondogo uwa tunaangalia tunatengeneza sh ngapi kwa Wanaotuuzia wengi na sio mtu mmoja. Hakikisha unakuwa na Center zaidi ya Moja ya Mauzo, Hapo ndipo utaona kama unatengeneza Faida ndefu.
3. STAND ZA MABASI/ FOLENI ZA MAGARI
Najua hata wewe ni mmoja ya wadau waliokwisha wahi nunua Eidha Maji au Kitu chochote ukiwa kwenye Gari wakati muuzaji yupo nje ya Gari akitembeza. Lakini Pia wapo wale wanaouza kwenye Stand yaani wanaweka Meza ikiwa na Vyakula Vikavu kibao.
Tambi za Dengu, pia uwa sehemu ya Bidhaa izo, Soko hili upokea Tambi za Dengu kwa Bei ya Jumla na Rejareja. Wakati fulani nikiwa pale Makumbusho nilikutana na Kijana Mmoja anaitwa Kiba, Kiba aliniambia Tambi za Dengu utoka sana katika Eneo la Makumbusho stand na wenyewe ununua Tambi zile kwa Mama mmoja ambaye anasambaza karibia Kwa Vijana wengi wenye Meza Pale Makumbusho.
Wakati namuuliza kama naweza kupeleka za kwangu, Jibu lake lilikuwa "Brother zikiwa Bora Zitachukuliwa zote na Wadau hapa". So kumbe ishu ni Ubora, Basi Kijana wangu ndani ya Zingo Products Bwana Baloz akadili na Kiba kibiashara zaidi.
Sehemu hii ya Stand za Magari ni Sehemu inayokuwa na Watu wengi sana wanaoingia na Kutoka..
Hivyo basi, tafuta masoko kulingana na eneo ulilopo, na angalia unatumiaje fursa zilizopo mbele yako ...KUTOBOA.
Una maoni gani juu ya hili??... #Shareshare
iko vizuri sana ila je kwenye ma supermarket soko lake lipoje?
JibuFuta