Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Njia 3 rahisi :Jinsi ya kutumia Facebook kutangaza na kukuza biashara yako

Ebu jiulize Leo, umeingia Facebook kwa mda gani?.. Asubuhi, mchana au jioni?

Well, tafiti zinasema watu wengi hawana muda maalum, muda wowote akiwa free na simu yake, tayari ashaingia Facebook.

Mfano rahisi tu, cheki kwenye daladala watu walioshika smartphone zao, huwezi kukosa ambao hawapo Facebook kwa muda huo.
Au ingia Facebook ktk account yako, anytime lazima ukute watu wapo online, (jaribu hata sasa hivi !!)

STORI ya hapo juu, ni funzo moja muhimu sana ambalo kama mfanyabiashara  au mjasiriamali wa karne hii ya teknolojia lazima ulifahamu.

Na funzo lenyewe ni kutambua ATTENTION ya wateja wako wa sasa, na wa baadae walipo...na si sehemu nyingine unayoweza kuwafikia kiurahisi kama kupitia mitandao ya kijamii, yaani Facebook, Instagram, WhatsApp, Snapchat, YouTube n.k

Kupitia social media, unao uwezo wa kufanya biashara yako 24hrs, kuongeza mipaka ya sehemu biashara yako inapoweza kufika...na hivyo kuleta faida kubwa sana kwako kama ukiitumia ipasavyo.

Kuna stori kibao jinsi watu wanavyoweza kufanya hivyo, mojawapo ilikua Jamii forum,mpiga picha aliyetengeza million 8 kupitia Instagram TU.,

Well, twende pamoja katika njia 3 unazoweza kutumia mtandao wa Facebook, kwa lengo la kutangaza biashara yako...



1. Tumia Profile yako kujitangaza

Facebook inakusaidia kupata marafiki,(mpaka 5000). Kati ya hawa wote, ni lazima utaweza kupata baadhi ambao wanaweza kuwa wateja wako,

Katika posti zako, ukiachana na zinazohusu maisha yako..tumia pia kuposti juu ya biashara unayofanya...toa mawasiliano yako.

Wateja walio interested watakutafuta, tumia hao ili kupata wengine wengi..

2. Tumia magroup ya biashara ya FB

Facebook (FB) inayo magroup kwa ajili ya kutangaza bidhaa, biashara.. Tena ya kwetu kabisa, kwa nini usiyatumie??

Mimi nshawahi fanya zoezi moja dogo sana, ila lina funzo kubwa ndani yake. Nlienda kariakoo, nikapiga picha za zile simple za kiume wanazouza elfu 12, picha zangu 3...nkaziposti katika group moja..nkaandika bei 15,000.  watu zaidi ya 20 walikomenti kuhitaji,.. Nkasema haah!...kumbe inawezekana bana.

Vipi sasa kwa biashara yako? Bidhaa zako za ujasiriamali??... Kuna positive impact kubwa sana unayoweza kuiongeza katika biashara yako kwa kuitangaza ktk magroup ya kuuza na kununua ya Facebook, kwa hapa Tz.

3.  Kuwa na official page ya biashara yako.

Hapa sasa, umeamua kuwa serious zaidi na kuiweka biashara yako online, unda Facebook page kwa ajili hii.

Kuwa na page, kutakusaidia kuijenga biashara yako, hasa katika branding na pia kupata wateja wengi baadae...ukishafahamika.
Page itakusaidia kuwajua vizuri zaidi wateja wako(kupitia analytics), na pia itakupa NAFASI adhimu ya kutangaza kupitia Facebook wenyewe (Facebook ads) .

Facebook ads/advertising ni mada kubwa na muhimu Sana kwako , tutaijadili kwa kina katika makala nyingi zinazokuja...
STAY TUNED....

#SHARE article hii iwafikie wengi zaidi...utakua umesaidia Sana

Tembelea Leo www.tanpreneurs.blogspot.com

Blog ya TZ kwa ajili yako mjasiriamali, mfanyabiashara au unayetaman kufanya shughuli hizo

Tunaamini ktk practical entrepreneurship,

Cc : *Tanzanian entrepreneurs* 🇹🇿🇹🇿

Maoni

  1. Nataka nifungue account ya biashara

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

BIASHARA YA CRIPS, ANZA LEO KWA MTAJI WA 50,000.

BIASHARA YA CRIPS....PART 1 Biashara ya Crips ni Biashara unayoweza sema ni Ndogo kama utawekeza kwa Udogo lakini pia unaweza sema ni ya kati kama utawekeza kwa ukati wake. Hii ni biashara ambayo mtu anaweza kuwekeza kwa kua na sh 50,000. Ndio Mtaji wa Elfu Hamsini unatosha kabisa kumfanya mtu aianze Biashara hii. Mtu anaweza Sema Inakuaje Elfu hamsini Ikawa Mtaji, Ni Hivi Katika 50000. Toa 20000 ya Mashine, Kisha Toa 12000 Ya Debe Moja la Viazi kisha toa 10500 ya Lita 3 za Mafuta , Kisha toa 2000 Ya Mkaa na Utoe pesa Ya Vifuko ni Sh 1200 vya kufungia na Chumvi 300 na Pilipili ya unga 500. Wataalamu wa Hesabu, ukipiga haizidi elfu 50. Halafu watu wapo mtaani wanalalamika hawana Mitaji,wanaishia kubeti, mara biko, tatu mzuka.. Kumbe mitaji yao wanachangia kwenye Harusi na Sendoff.  Embu jiulize umeua Mitaji mingapi kwa kuchangia Harusi na Sendoff, kubeti, kucheza biko/tatu mzuka au kununulia nguo ya Sherehe alafu kesho yake unapiga mihayo na kusema Vyuma Vimekaza. H

Jinsi ya kupika crips (mwanzo hadi mwisho)

MAHITAJI YA KUPIKA CRIPS ZA VIAZI ü   Viazi ü   Mafuta ya Kula ü   Chumvi Au Pilipili ya Unga ü   Mashine ya Kukatia ü   Moto na Vyombo vya kupikia. HATUA ZA UPISHI WA CRIPS ZA Viazi Kwanza menya Viazi vyako na Viweke Kwenye Maji ambapo vitaoshwa. Chukua Mashine yako ya Kukatia na Ioshe na Maji kwanza. Kata kwanza Viazi vyako ili viweze kuwa kama Vipande viitwavyo Crips. Weka Mafuta kwenye Moto na hakikisha moto wako unawaka vizuri. Hakikisha Wakati unakata Viazi vyako vidondokee kwenye maji ili visigandane. Hakikisha mafuta yanapata moto ndio uweke Crips zako humo. Subiria kaa muda wa Dakika 7 hadi 10 kisha Geuza na baada ya muda mchache crips zako zitakuwa zimesha iva. Ipua na uweke kwenye chujio la Kuchuja mafuta. Hakikisha mafuta yanachujwa na crips iwe kavu ili wakati unaweka kwenye vifuko isitengeneze Umafuta ndani yake itakera. Weka Kwenye Besen kisha weka chumvi kwa Mbali na upepete ili ichanganyik

JINSI YA KUKUZA BIASHARA NDOGO: Mambo 6 ya kuzingatia...(part 2)

Huu ni mwendelezo wa makala yetu iliyopita, tuna endelea na jambo la 4 #4. Kuhakikisha unatengeneza mtandao wako wa kukuza soko lako Tambua kuwa biashara hizi ndogo ndogo mara nyingi faida zake si kubwa sana lakini zina faida endapo utakua na masoko mengi tofauti tofauti. Na maanisha nini?? Usiwe unapika Crips ukataka uishie kuuza wewe mwenyewe au ukaishia kuuzia hapo kibarazani kwako Hakikisha unakuwa na waru wengine ambao watanunua kwako bidhaa hata kwa jumla na wao kwenda kuziuza au lah uwe na sehemu nyingi za kwenda kuuzia bidhaa zako. Unapika vitafunwa usiishie kuuza hapo kibarazani kwako, badala yake ongea na viduka vya Mangi waachie vitafunwa vyako hapo wakuuzie au uwauzie kwa jumlan tengeneza vingine tafuta sehemu zingine za kwenda kuuza kama ni maofisin, stendi, sehemu zenye msongamano wa watu, mahotelini au migahawani, nk ili soko lako liwe kubwa kusudi ukikusanya hizo mia mbili au mia tano sehemu nyingi zaidi zikuletee faida nzuri vinginevyo kwa kutegemea soko