Ruka hadi kwenye maudhui makuu

JINSI YA KUKUZA BIASHARA NDOGO: Mambo 6 ya kuzingatia...(part 2)

Huu ni mwendelezo wa makala yetu iliyopita, tuna endelea na jambo la 4



#4. Kuhakikisha unatengeneza mtandao wako wa kukuza soko lako

Tambua kuwa biashara hizi ndogo ndogo mara nyingi faida zake si kubwa sana lakini zina faida endapo utakua na masoko mengi tofauti tofauti.

Na maanisha nini??
Usiwe unapika Crips ukataka uishie kuuza wewe mwenyewe au ukaishia kuuzia hapo kibarazani kwako

Hakikisha unakuwa na waru wengine ambao watanunua kwako bidhaa hata kwa jumla na wao kwenda kuziuza au lah uwe na sehemu nyingi za kwenda kuuzia bidhaa zako.

Unapika vitafunwa usiishie kuuza hapo kibarazani kwako, badala yake ongea na viduka vya Mangi waachie vitafunwa vyako hapo wakuuzie au uwauzie kwa jumlan tengeneza vingine tafuta sehemu zingine za kwenda kuuza kama ni maofisin, stendi, sehemu zenye msongamano wa watu, mahotelini au migahawani, nk ili soko lako liwe kubwa kusudi ukikusanya hizo mia mbili au mia tano sehemu nyingi zaidi zikuletee faida nzuri vinginevyo kwa kutegemea soko moja biashara inaweza ikakudodea


#5. Kutumia njia za bure za kutangaza biashara yako

Pamoja na kuwaambia wanaokujua kuhusu biashara yako, bado unahitaji kutumia njia nyingine kutangaza biashara yako, lakini kwa kuwa wewe unaanza na mtaji kidogo, huwezi kumudu gharama kubwa za matangazo ya televisheni, redio au magazeti.

Lakini kukosa haya bado kuna njia nyingi sana za kutangaza biashara yako bure.
Mfano unaweza kutumia mitandao ya kijamii kutangaza biashara yako au makundi yako ya whatsapp uliyonayo sio tu kupoteza bando kuchat umbea huku ikiwa una makundi 20 ya whatsapp lakini hakuna anaejua kuwa unauza karanga au ubuyu au crips

Pia tumia nafasi za kijamii kuitangaza biashara yako mfano ikitokea umeenda kwenye kikao fulani beba bidhaa zako weka kwenye mfuko kauze huko, sijui kuna semina umeenda beba bidhaa zako kajitangaze hata usipouza lakini kuna watu utakuwa umewafikia na wamejua kuwa unauza bidhaa fulani

Tukumbuke kuwa "Hakuna Biashara bila wateja, na biashara ni matangazo"

 hivyo tafuta njia mbadala za kujitangaza ambazo hazitohusisha wewe kulipia gharama kubwa ili hali una mtaji mdogo



#6. Kuhakikisha unajitoa kufanya kazi sana

Biashara inahitaji ujitoe kufanya kazi.

Lakini tambua kuwa ukianzisha biashara na mtaji mdogo ina maana sehemu kubwa ya kazi katika biashara yako ni lazima utahusika nayo wewe mwenyewe utake usitake.

Hivyo biashara unayoanza kwa mtaji kidogo inahitaji ujitoe hasa, sio kidogo.

Kwanza utafanya majukumu mengi kwa wakati mmoja.
Wewe ndio utakuwa mfataji malighafi sokoni, wewe utakuwa pengine ndio mzalishaji au mtengenezaji, wewe ndio utajiita Afisa Masoko hahahahaha, wewe ndio utakuwa Muhasibu, wewe ndio utakuwa mtu wa huduma kwa wateja na mengine mengi.

Majukumu yote haya yanahitaji wewe kujitoa na kuweka kazi kubwa ili kuweza kuikuza biashara yako.
Jiandae kwa kazi ya kutosha na kuwa tayari kujitoa, hili ni tegemeo kubwa sana kwenye biashara yako.

Usitake kujiita CEO ili hali hujitumi kwenye biashara yako, kumbuka kwa wakati huo unaweza usiwe hata na uwezo wa kuajiri kijana japo mmoja wa kukusaidia hivyo utahitajika ujitoe haswa, utasweti sana, utatoka jasho sana, utaungua sana, utafubaa na moshi lakini inabidi iwe hivyo ili hiyo biashara yako itoke hapo kuwa ndogo mpaka ufikie hatua ya kuweza kuajiri watu wa kufanya kazi kwa niaba yako la sivyo biashara itadorola au itafia mikononi mwako

Nimalizie tu kwa kusema kwamba:

Kuwa na mtaji kidogo kunatosha kuiwezesha ndoto yako ya kuwa na biashara kubwa.

Kuwa na mtaji mdogo kunaweza kukufanya ukamiliki biashara yako bila shida.

Kuwa na mtaji mdogo haimaanishi kuwa biashara yako itafeli

Kumbuka hata hao matajiri wakubwa licha ya kuwa na mabilionea ya fedha lakini leo hii wakitaka kujenga ghorofa itawalazimu waanzie chini hivyo wewe kwa kuanzia chini na mtaji mdogo basi jua kuwa unajitengenezea msingi mzuri wa biashara yako siku zijazo.

Fanya mambo hayo sita na biashara yako itakuwa kubwa na yenye mafanikio,

Ahsante na karibu tena ktk blog hii kwa makala za ujasiriamali na biashara zenye uhalisia #practical entrepreneurship

Toa maoni yako na usisahau kushea

Maoni

  1. Safi Sana ndugu nimependa vile unatuamasisha kujitoa# vijana tusilale kumekucha

    JibuFuta
  2. Daa unajua xn!! kuchambua maswala mazma ya biashara yaan (@) umenipa myo(b) ujasili(c) umakini(na kujiamini pia na nimeziandka points muhimu ebwna mm nitaendelea kukufwatlia p1 xn

    JibuFuta
  3. Thanks San Kwa ushauri mzur na wenye ladha kinywani na unao ingia akilini 🤝

    JibuFuta
  4. Mungu akubariki sana naomba kuuliza ni aina gani ya viazi inafaa kupikia clips

    JibuFuta
  5. Asante kuna kitu nimepata

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

BIASHARA YA CRIPS, ANZA LEO KWA MTAJI WA 50,000.

BIASHARA YA CRIPS....PART 1 Biashara ya Crips ni Biashara unayoweza sema ni Ndogo kama utawekeza kwa Udogo lakini pia unaweza sema ni ya kati kama utawekeza kwa ukati wake. Hii ni biashara ambayo mtu anaweza kuwekeza kwa kua na sh 50,000. Ndio Mtaji wa Elfu Hamsini unatosha kabisa kumfanya mtu aianze Biashara hii. Mtu anaweza Sema Inakuaje Elfu hamsini Ikawa Mtaji, Ni Hivi Katika 50000. Toa 20000 ya Mashine, Kisha Toa 12000 Ya Debe Moja la Viazi kisha toa 10500 ya Lita 3 za Mafuta , Kisha toa 2000 Ya Mkaa na Utoe pesa Ya Vifuko ni Sh 1200 vya kufungia na Chumvi 300 na Pilipili ya unga 500. Wataalamu wa Hesabu, ukipiga haizidi elfu 50. Halafu watu wapo mtaani wanalalamika hawana Mitaji,wanaishia kubeti, mara biko, tatu mzuka.. Kumbe mitaji yao wanachangia kwenye Harusi na Sendoff.  Embu jiulize umeua Mitaji mingapi kwa kuchangia Harusi na Sendoff, kubeti, kucheza biko/tatu mzuka au kununulia nguo ya Sherehe alafu kesho yake unapiga mihayo na kusema Vyuma Vimekaza. H

Jinsi ya kupika crips (mwanzo hadi mwisho)

MAHITAJI YA KUPIKA CRIPS ZA VIAZI ü   Viazi ü   Mafuta ya Kula ü   Chumvi Au Pilipili ya Unga ü   Mashine ya Kukatia ü   Moto na Vyombo vya kupikia. HATUA ZA UPISHI WA CRIPS ZA Viazi Kwanza menya Viazi vyako na Viweke Kwenye Maji ambapo vitaoshwa. Chukua Mashine yako ya Kukatia na Ioshe na Maji kwanza. Kata kwanza Viazi vyako ili viweze kuwa kama Vipande viitwavyo Crips. Weka Mafuta kwenye Moto na hakikisha moto wako unawaka vizuri. Hakikisha Wakati unakata Viazi vyako vidondokee kwenye maji ili visigandane. Hakikisha mafuta yanapata moto ndio uweke Crips zako humo. Subiria kaa muda wa Dakika 7 hadi 10 kisha Geuza na baada ya muda mchache crips zako zitakuwa zimesha iva. Ipua na uweke kwenye chujio la Kuchuja mafuta. Hakikisha mafuta yanachujwa na crips iwe kavu ili wakati unaweka kwenye vifuko isitengeneze Umafuta ndani yake itakera. Weka Kwenye Besen kisha weka chumvi kwa Mbali na upepete ili ichanganyik