Katika kutambua fursa za kibiashara, ni lazima ujue kufanya utafiti mzuri wa masoko,..jifunze kitu katika stori hii ya kweli kutoka kwa mjasiriamali mmoja..
"Katika pita pita zangu leo nikakutana na muuza crisps
Nikasema wacha nimuungishe mjasiriamali mwenzangu huku tukipiga stori za hapa na pale.........
Kwanza nilianza kwa kumuuliza bei ya crisp na kisha nikampa hela na kununua ili niweze kubonga nae stor vizuri maana asikwambie mtu, ni ngumu kumdadisi mfanyabiashara ikiwa hamjazoeana wala hamfahamiani.
Mtu anaweza akahisi unamchawia au unamletea nuksi au pengine unataka na wewe uje ufungie biashara kama hyo halafu uishie kuwa mshindani wake
Nikanunua pakiti yangu nikawa nakula mdogo mdogo huku nikianza kupuga nae stori.
Nilimuanzia mbali sana ili kuepuka kumfanya ashindwe kuniweka bayana juu ya hiyo biashara yake.
Nilianza kwa kumuelezea juu ya biashara yangu ya karanga na changamoto zake baada ya Diamond Karanga kuibuka (huku nikiwa hata sijawai fanya biashara ya karanga 🤣🤣 ila tu inabidi kunogesha maongez ili kupata taarifa sahihi unazohitaji)
Ndipo akaniambia ni kweli hata mie bosi wangu alikuwa akifanya hiyo biashara ila sasa hivi analalamika biashara hiyo haitoki sana tofauti na biashara yake nyingine.
Ndipo nikaanza kumuuliza ni biashara ipi nyingine ambayo boss anafanya??
Ndipo akaniambia kuwa bosi wake anatengeneza Crisp za aina tofaut tofaut na kuziuza
Kusikia hvyo nikaona eeewaaa sasa amekuja kwenye mstari ninaouhitaji.
Basi nikaanza muhoji anatengeneza crisp zip na zip akanitajia kijana wa watu bila hiyana (nikaona kagusa mule mule kwenye biashara zetu za crisp tulizojifunza)
Nikazid kumpeleleza kijana kuhusu anavyoiona hyo biashara ya crisp je zinatoka tofaut na karanga??
Akaniambia yah zinatoka sana hasa maeneo ya stendi ambapo yeye yupo lakini hata kwenye hizi foleni za daladala zinauzika sana maana unakuta mtu ana njaa au anataman kutafuna ktu akikuona anakuita na kununua
Nilienda mbal zaidi kumuuliza sasa je wewe huyo boss wako anakulipa kiasi gan kwa mwezi??
Akaniambia mie silipwi kwa mwezi ila naumbulia Sh 300/= tu kwa kila mfuko ninaouza ambapo mfuko huko yeye anauuza kwa Sh 1,000/=
Akaniambia huyo boss wao yeye mwenyewe anatengeneza, kupack na kuwauzia vijana tofaut tofaut kwa Sh 700/= kwa pakiti kubwa na Sh 400/= kwa ile pakiti saizi ya kati
Kwa hiyo wao wanakuja kuziuza kwa Sh 500 (zile za 400 na kupata sh 100 yao) na zile za 700 wanauza kwa Sh 1000 wanapata cha kwao sh 300
Ndipo nikakumbuka maneno ya mkufunzi wetu hapa kuwa tengeneza soko lako kubwa kwa kuwauzia watu wengi tofaut tofauti bidhaa zako ili kuweza kukuza soko lako lakini pia kuufanya mzunguko wa biashara yako kuwa mkubwa zaidi siku hadi siku
Kweli nimeamini kuna nguvu kubwa katika kuwa na mawakala au wasambazaji au wauzaji wa bidhaa zako kwani pengine kwa wewe mwenyewe ungeweza kuziuza bidhaa zako si ajabu sehemu tu ile uliyopo lakini pengine ukiwa na wasambazaji wengi zaidi kwa hakika bidhaa zako zitafika sehemu kubwa zaidi
Usitake kung'ang'ania faida yote ije kwako ili hali bidhaa zako zinaweza chukua muda mrefu sana hadi kuja kuuzika zote wakati kumbe ungepata wasambazaji au mawakala wa bidhaa zako zingekuwa zikitoka kwa wingi sana na hvyo kukupa faida mara dufu
Kwa hyo tunajifunza nini kupitia mfano huu??
1. Kwanza tunapoenda kwa wafanyabiashara usikurupuke moja kwa moja kuanza kumuuliza maswali yanayoihusu biashara yake kwani ni wazi kuwa mtu asiekufahamu hawezi kukupa taarifa za biashara anayoifanya kirahisi rahisi aidha kwa kuhofia usije kuwa mshindani wake kesho yake au kukupa siri kuhusu biashara yake
2. Ili biashara yako ikue tengeneza jina zuri la biashara yako, fanya bidhaa zako zikubalike na kuhitajika kwa kiasi kikubwa aidha kutokana na ubora wake, nk
3. Ukishakuza jina lako, tafuta mawakala, wasambazaji au wauzaji wa bidhaa zako sehemu zingine ili kuzidi kukuza biashara yako zaidi
4. Usitake faida yote uitafune mwenyewe, jaribu kuangalia namna ya kugawana na wengine ili kukuza mzunguko wako wa biashara.
Ukiwa na watu 10 wanaouza bidhaa zako ni tofaut sana na ukiwa peke yako ndio unaeuza
Tuangalie watu kama kina Bakharesa, Mo Dewji wanavyosambaza bidhaa zao kwenye viduka vya maduka, walivyo na mawakala unakuta hata watu wanaokuja kununua bidhaa kwako ni wengi na wanachukua mzigo mkubwa mkubwa tofaut na akija mtu mmoja kununua bidhaa yako.
Kwa kumalizia tu niseme kuwa biashara yako inajengwa na kukuzwa na wewe mwenyewe, namna utakavyoijenga ndivyo itakavyokua.
Namna utakavyotumia muda wako mwingi kuijenga na kuiboresha na kufanya vitu vya kubuni kila siku ndivyo itakavyokua.
Wewe usipoipa muda wa kutosha hakika itakufa kwani maono ya kwako wewe kama muanzilishi ni tofaut sana na yule utakaemuajiri hata kama utamlipa vizuri
Yap ni kweli.
Kuna wafanyabiashara anaona kuliko nisubiri faida ya elfu 10 niile mwenyewe wakati itachukua muda mrefu kuja kuipata ni heri apate faida elfu 3 lakini iwe inakuja kwa haraka zaidi
Mzunguko wa Biashara wa haraka zaidi ni bora sana katika biashara zetu , hasa biashara ndogo ndogo.
Maoni
Chapisha Maoni