Ruka hadi kwenye maudhui makuu

BIASHARA YA CRIPS, ANZA LEO KWA MTAJI WA 50,000.

BIASHARA YA CRIPS....PART 1

Biashara ya Crips ni Biashara unayoweza sema ni Ndogo kama utawekeza kwa Udogo lakini pia unaweza sema ni ya kati kama utawekeza kwa ukati wake. Hii ni biashara ambayo mtu anaweza kuwekeza kwa kua na sh 50,000. Ndio Mtaji wa Elfu Hamsini unatosha kabisa kumfanya mtu aianze Biashara hii.



Mtu anaweza Sema Inakuaje Elfu hamsini Ikawa Mtaji, Ni Hivi Katika 50000. Toa 20000 ya Mashine, Kisha Toa 12000 Ya Debe Moja la Viazi kisha toa 10500 ya Lita 3 za Mafuta , Kisha toa 2000 Ya Mkaa na Utoe pesa Ya Vifuko ni Sh 1200 vya kufungia na Chumvi 300 na Pilipili ya unga 500. Wataalamu wa Hesabu, ukipiga haizidi elfu 50.

Halafu watu wapo mtaani wanalalamika hawana Mitaji,wanaishia kubeti, mara biko, tatu mzuka.. Kumbe mitaji yao wanachangia kwenye Harusi na Sendoff.
 Embu jiulize umeua Mitaji mingapi kwa kuchangia Harusi na Sendoff, kubeti, kucheza biko/tatu mzuka au kununulia nguo ya Sherehe alafu kesho yake unapiga mihayo na kusema Vyuma Vimekaza. Haahaahaa Daah! Elfu Hamsini tu inaweza kukubadilishia Mchakato wa kukaza kwa Vyuma.

Na Endapo Utapanua Soko unaweza kujikuta unasogea kimaisha. Wakati fulani niliwahi kujikita kutafiti soko la Crips katika stand mbalimbali za Magari, Nilikutana na mambo nisiyoyategemea. Vijana wale wauzaji wa Pale Makumbusho Stand waliniambia wananunua Crips kwa Bei ya Jumla kwa sh 450 kwa Crips inayouzwa 500. Pia kabla ijaondoka Mmoja akaniita "Brother ziwe na Ubora Tu, sisi tunanunua". Hapa ndipo nilipomwambia kijana wangu Mwasha, Hapa kuna soko Huria. Yaani gombania Goli.

Hizi Biashara za Crips zimegawanyika katika Sehemu Tatu, Zipo za Viazi, Mihogo na Ndizi.
Mfano ulioniacha mdomo wazi, Mkungu mmoja wa Mzuzu ambawo unauzwa 15000-20000 Unaweza kutoa Crips za 1000 Pic 50. Si moja nikiwa Tazara nilikutana na kijana #Joseph, Kijana mzoefu katika uuzaji wa Crips katika Foleni ya Tazara. Nilikaa na kuzungumza nae kwa Muda wa Dak 30  na yeye alinipa Fact nyingi kuhusu Biashara hii ya Crips za Ndizi. Aliniambia Mkungu mmoja wa Mzuzu yeye uweza kupata Pic 50 za 1000

Hapa niliwaza kama nina vijana kama Joseph katika Trafic Jam 10 Hapa Dar Es Salaam nitakuwa wapi baada ya Mwaka mmoja... Nilinyanyua simu na Kumpigia kijana wangu wa Masoko bwana Mwasha na kumwambia 'Tusichelewe'.

ITAENDELEA… USIKOSE KUFATILIA
Toa maoni yako kuhusu biashara hii, je unaionaje??.....


Maoni

  1. Nmevutiwa sana na hii biashara na nmepata hamasa ya kufany biashara

    JibuFuta
  2. Mashine zinapatikana wapi

    JibuFuta
  3. Asante sana kwa mafunzo hayo mazuri Mimi nilianza kwa kiasi kidogo sana shs 20,000 tu Na ninaendelea na sasa nimeanza kupataorder. Biashara nzuri.

    JibuFuta
  4. Waooooo nimefurah sanaaaa.. na nimepata new idea na nguvu ya kuzidi kukifanya kile nilichokuwa nakifikiria... Barikiwa sanaaa.

    JibuFuta
  5. Ni wazo zuri ni wapi wanapatikana kwa dodoma??

    JibuFuta
  6. Mashine bei yake ni elf 20, mbona nimeiyona sehem wanasema elf 85

    JibuFuta
  7. mashine zimejaa kaliakoo kuanzia elfu kumi mpaka elfu kumi na tano , hata mie nimenunua last week kupeleka kigoma.

    JibuFuta
  8. mashine si hizi ndogo zinauzwa au hiyoya elf 20 ikoje nimependa maelezo yako

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Jinsi ya kupika crips (mwanzo hadi mwisho)

MAHITAJI YA KUPIKA CRIPS ZA VIAZI ü   Viazi ü   Mafuta ya Kula ü   Chumvi Au Pilipili ya Unga ü   Mashine ya Kukatia ü   Moto na Vyombo vya kupikia. HATUA ZA UPISHI WA CRIPS ZA Viazi Kwanza menya Viazi vyako na Viweke Kwenye Maji ambapo vitaoshwa. Chukua Mashine yako ya Kukatia na Ioshe na Maji kwanza. Kata kwanza Viazi vyako ili viweze kuwa kama Vipande viitwavyo Crips. Weka Mafuta kwenye Moto na hakikisha moto wako unawaka vizuri. Hakikisha Wakati unakata Viazi vyako vidondokee kwenye maji ili visigandane. Hakikisha mafuta yanapata moto ndio uweke Crips zako humo. Subiria kaa muda wa Dakika 7 hadi 10 kisha Geuza na baada ya muda mchache crips zako zitakuwa zimesha iva. Ipua na uweke kwenye chujio la Kuchuja mafuta. Hakikisha mafuta yanachujwa na crips iwe kavu ili wakati unaweka kwenye vifuko isitengeneze Umafuta ndani yake itakera. Weka Kwenye Besen kisha weka chumvi kwa Mbali na...

Mifano halisi: Masoko ya bidhaa zako za ujasiriamali (crips,tambi)

1.SHULENI (hasa za msingi) Kama ilivyo katika biashara ya Crips, Shule za Misingi pia ni Soko la Tambi za Dengu. Hapa katika Shule za Misingi pia kuna upenyo wa kufanya Biashara hii kwa kuuza Mwenyewe au kuwapa Vijana wakuuzie au kuwaomba wale wanaouza Vipipi wakuuzie kwa Kutengeneza Mgawanyo wa Pato la Kila bidhaa moja. Mfano Bidhaa ya Sh 200, Wewe mpe mtu uyo auze kisha mwambie achukue sh 40 na wewe utapata 160. Mara zote nasema Chukua kidogokidogo kwa Wengi, Nikimaanisha Kama utapeleka bidhaa zako katika shule 10 na kupata Faida ya Sh 50 kwenye Kila bidhaa moja na wewe umepeleka bidhaa 100 kila shule. Maana yake utakuwa umetengeneza Faida ya 5000 Mara shule 10 utakuwa na 50,000 kwa Siku hii. Tambi za Dengu zinalika Pia shule za Misingi. 2.MADUKA YA MTAANI Maduka ya Mitaani ni sehemu ya Soko la Tambi za Dengu. Je Mtaani kwako kuna Maduka Mangapi, Je Maduka yaliochangamka ni mangapi? Je Maduka gani yanamuingiliano wa Watu sana. Jambo la Msingi hapa Ni kuangalia Maduka Yaliyocha...